RASMI; Klabu ya Manchester City imekamilisha usajili wa Mateo Kovacic kutokea Chelsea Jumanne Wiki hii. Amesaini mkataba wenye thamani ya Pauni Milioni 25 ($ 31.9m) wa kuitumikia Klabu hio kwa muda wa Miaka minne.
Mkataba mpya wa nyota huyo wa Croatia utamweka Etihad hadi msimu wa joto wa 2027, na tangazo la Jumanne jioni linamfanya kuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa na klabu hiyo kwenye dirisha hili.
Mabingwa hao wa Uingereza walianza mazungumzo na wapinzani wao wa Ligi Kuu mwanzoni mwa Juni, kabla ya majukumu ya Kovacic ya kimataifa.