ADVERTISEMENT
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
Tuesday, October 3, 2023
  • Login
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
No Result
View All Result

MWANASHERIA MKUU AJITOSA MJADALA WA UWEKEZAJI WA DP WORLD

Dodoma

MTEWELE ALFRED by MTEWELE ALFRED
Jun 27, 2023
in HABARI
0
MWANASHERIA MKUU AJITOSA MJADALA WA UWEKEZAJI WA DP WORLD
0
SHARES
79
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

AG Feleshi tells legal service providers to embrace values - Daily NewsMwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Dkt. Eliezer Feleshi, amejitosa kwenye mjadala wa uwekezaji wa kampuni ya Dubai ya DP World unaotarajiwa kufanywa kwenye bandari ya Dar es Salaam kwa kusema kuwa kuna upotoshaji mkubwa usio na tija katika mjadala huo.

Akizungumza kwa mara ya kwanza katika mahojiano maalumu ofisini kwake Dodoma, Jaji Feleshi amesema kuwa upotoshaji huo unaweza kuifanya Tanzania ionekane kama inabagua wawekezaji kutoka nchi fulani.

RelatedPosts

MAHAKAMA YATHIBITISHA MKATABA UWEKEZAJI BANDARI KISHERIA

MAHAKAMA YATHIBITISHA MKATABA UWEKEZAJI BANDARI KISHERIA

Aug 11, 2023

WAZIRI AWESO AZINDUA MRADI WA MAJI KALIUA, TABORA

Aug 1, 2023

ZAIDI YA BIL. 31 KUTUMIKA KUKARABATI UWANJA WA MKAPA

Jul 28, 2023
Load More

“Mtu anasema mkataba ni wa miaka 100 na hiyo ilikuja hata kabla Bunge halijaazimia. Wengine wanasema ni mkataba wa maisha. Unatafuta hicho kipengele cha maisha unapekua kifungu kimoja mpaka mwisho, hakuna,” alisema Feleshi.

Ameonya pia kuwa lugha za kibaguzi zinazotolewa na baadhi ya watu dhidi ya wawekezaji kutoka nchi fulani zinaweza kuharibu sifa ya Tanzania kama taifa linaloongoza kuvutia watalii kwenye ukanda huu wa Afrika.

“Je sasa tunataka tujenge mazingira ya kuwatia hofu wawekezaji kwamba nchi yetu haitaki wawekezaji?” Alihoji Jaji Feleshi. Aliongeza kuwa Tanzania imekuwa inajulikana kama nchi ambayo haifungamani na upande wowote miaka mingi na inayokaribisha wawekezaji kutoka sehemu zote duniani.

“Leo unapoanza kuona Waarabu ni kama shida, unachagua (wawekezaji watoke) wapi?” Aliongeza. Mwanasheria Mkuu wa Serikali pia amepangua upotoshaji kuwa bandari ya Dar es Salaam inauzwa kwa kusema kuwa hakuna kipengele chochote kwenye mkataba kati ya Tanzania na Dubai (intergovernmental agreement au IGA) kinachozungumzia uuzwaji wa Bandari.

“Tunaposema bandari imeuzwa, je ni kweli imeuzwa? Kile kiambatisho kimeeleza maeneo ya mahusiano kwa mujibu wa ile ibara ya 4 ni kwenye gati ngapi kati ya ngapi na hizo zinazobaki ni ngapi,” alisisitiza. Alifafanua kuwa Bunge limepitisha azimio la Ushirikiano kati ya Serikali ya Dubai na Tanzania kwenye eneo la bandari, lakini hakuna mkataba wowote ambao umesainiwa kati ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) na Kampuni ya DP World.

“Mpaka sasa TPA haijaingia makubaliano au mkataba wowote na DP World kwani muda wake haujafika,” alisema. Alikanusa upotoshaji unaonezwa na baadhi ya watu kuwa Tanzania au TPA haitaweza kujitoa katika makubaliano itakayoingia na DP World.

“Kama kuna kushindwana framework (msingi) umeshawekwa. Tangu mwanzo kwenye preamble (utangulizi wa makubaliano) imetajwa mikataba itakayokuja kuingiwa kama HGA (host government agreement) na project agreement (mtakaba wa uendeshaji wa magati ya bandari),” alisema.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali ameongeza kuwa katika mkataba ambao TPA itasaini na DP World, mwekezaji huyo atapewa masharti mahsusi na malengo ya utendaji na endapo mwekezaji ataonesha ufanisi, ataweza kuongezewa maeneo mengine kwa mujibu wa matakwa ya serikali.

Feleshi, ambaye amewahi kuwa Mkurugenzi wa Mashitaka (DDP) na Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania

 Mwanasheria Mkuu wa Serikali Eliezer Feleshi Azungumzia Mjadala wa DP World

Achambua mkataba kati ya Dubai na Tanzania kipengele kwa kipengele

Apangua upotoshaji wa bandari kuuzwa, mkataba wa miaka 100 au maisha

Aonya kuhusu madhara ya kubagua wawekezaji kutoka nchi fulani

Asisitiza kuwa mpaka sasa TPA haijaingia mkataba wowote na DP World

Related

Tags: BANDARI YA DAR ES SALAAMDP WORLDIKULU MAWASILIANOWIZARA YA BIASHARA NA UWEKEZAJI
MTEWELE ALFRED

MTEWELE ALFRED

Related Posts

KANISA LAPOROMOKA MEXICO NA KUUWA WATU 10
HABARI

KANISA LAPOROMOKA MEXICO NA KUUWA WATU 10

by SUZO SHUKRANI
Oct 2, 2023
HABARI

TAKRIBAN WAHAMIAJI 10 WAMEFARIKI NA WENGINE 25 KUJERUHIWA KATIKA AJALI YA LORI NCHINI MEXICO

by SUZO SHUKRANI
Oct 2, 2023
AIRPORT YA ZANZIBAR IPO BUSY KULIKO YA DAR ES SALAAM
HABARI

AIRPORT YA ZANZIBAR IPO BUSY KULIKO YA DAR ES SALAAM

by SUZO SHUKRANI
Oct 2, 2023
MIFUMO YA KIFEDHA KULINDWA ZAIDI
BIASHARA

MIFUMO YA KIFEDHA KULINDWA ZAIDI

by SUZO SHUKRANI
Oct 2, 2023
SIKU 7 ZATOLEWA MILANGO KUBADILISHWA
HABARI

SIKU 7 ZATOLEWA MILANGO KUBADILISHWA

by SUZO SHUKRANI
Oct 2, 2023
TWENDE BUTIAMA YAANZA RASMI KUTOKA DAR MPAKA BUTIAMA
HABARI

TWENDE BUTIAMA YAANZA RASMI KUTOKA DAR MPAKA BUTIAMA

by SUZO SHUKRANI
Oct 2, 2023

KRANTZ MWANTEPELE (FOUNDER & CEO)

KONCEPT TV

https://www.youtube.com/watch?v=0HP0mB_rtIU&t=7s
KONCEPT TV

KONCEPT TWEETS

June 2023
M T W T F S S
 1234
567891011
12131415161718
19202122232425
2627282930  
« May   Jul »
Currently Playing
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In