Kupitia Kurugenzi ya Mawasiliano Ofisi ya Rais Ikulu imeripotiwa kuwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Dkt. Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi huu mpya kama ifuatavyo;
Amemteua Bw, Omar Issa kuwa Mkuu (Chancellor) wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela (NM-AIST).
Bw. Issa ni mwenyekiti wa Bodi ya TANESCO na anachukua nafasi ya Mhe. Dkt. Gharib Bilali, Makamu wa Rais Mstaafu ambaye amemaliza muda wake.
Amemteua Prof. Abel N, Makubikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mifupa (MOI). Prof. Makubi anachukua nafasi ya Dkt. respicious Boniface ambaye amemaliza muda wake.
Amemteua Dkt. Abdulhamid Yahya Mzee kuwa Mkuu wa Chuo (Chancellor) cha Taifa cha Ulinzi.
Anemteua Dkt. Edwin Mhede kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya NMB Plc kwa Kipindi cha Pili.
Uteuzi huu umeanza tarehe 06 Juni, 2023
#KoncepttvUpdates