Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Dkt. Samia Suluhu Hassan kupitia ukurasa wa mtandao wa kijamii wa Twitter ametoa salamu za pole kwa wanafamilia ya Mmiliki wa Shirika la Ndege la Precision Air Bwn. Michael N. Shirima kufuatia taarifa zilizotolewa kuhusu kuaga Dunia hapo jana usiku.
“Nimepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha Michael Ngaleku Shirima, mwanzilishi na Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Precision Air. Baada ya utumishi wake kwa umma, kwa zaidi ya miaka 30 amekuwa sehemu muhimu katika biashara ya anga na shughuli za kijamii katika nchi yetu. Natoa pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki. Mwenyezi Mungu amweke mahali pema. Amina.” @SuluhuSamia