Mamlaka ya Mapato Nchini, TRA imeujuza Umma kuwa Usajili wa TIN kwa Mwanchi mwenye umri kuanzia miaka 18 haiusihani na usajili wa Biashara bali ni kwaajili ya Utambuzi kama ambavyo ulivyo usajili wa kitambulisho cha Taifa (NIDA) unafanywa tu pale mtu anapotimiza umri wa utu uzima kisheria.
Twakwa hilo ni kwa mujibu wa mabadiliko ya kifungu cha 22 na Sheria ya Usimamizi wa Kodi yaliotokana na kifungu cha 106 cha Sheria ya Fedha ya 2022 ambapo mhusika ambaye hafanyi biashara hupewa TIN isiyo ya biashara (Non Business TIN) ambayo hata hivyo inaweza hitajika pale unapotaka kuomba leseni ya Udereva au kuajiriwa n.k
Ifahamike kuwa ukiwa na TIN isiyo ya biashara ,ukianza biashara utatakiwa kufika TRA iliyo karibu na Biashara ili iweze kuhusishwa na kupatiwa cheti cha TIN kwa ajili ya Biashara husika.
Kwa Maboresho TRA iliyoyafanya hivi karibuni, TIN inapatikana kwa njia ya mtandao bila malipo yoyote.
Aidha imependa kuwatoa wasiwasi na kusisitiza kuwa mwananchi asiyefanya biashara au shughuli yoyote yenye kipato hatotozwa kodi yoyote.