Serikali kupitia Wizara ya Nishati, Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji, EWURA, United Nations Development Programme UNDP na Shirika la Umeme nchini TANESCO wameendelea kupambania Kutekeleza Mpango wa Matumizi ya Nishati Mbadala wa Kimataifa kupunguza gharama za uendeshaji kwa kutumia nishati kwa kuhakikisha kunakuwa na utumiaji wa nishati mbadala kama ilivyo ya umeme ili kuleta tija kupitia teknolojia hio mpya.
Imeanza kutekeleza matumizi ya mfumo huo kwa kufungua vituo rasmi vya kuchajia Magari ya Umeme jijini Dodoma ambapo kwa hapo baadae unaweza kuchukua nafasi kuwepo nchi nzima.
Kwa sasa wamejikita zaidi kuweza wekeza katika mfumo huo ili kupunguza uunuzi na usafirishaji wa Dizeli na Petroli ambapo kwa usiku pindi maumizi ya umeme yanapokuwa chini Magari ya Umeme yanapata tena nafasi ya kuchajiwa na kuendelea kutumika ili kuendana na mabadiliko yanayojitokeza kila mara.Mwenyekiti wa Bodi ( wa tatu kulia) Prof. Mark Mwandosya akitizama namna gari inayotumia umeme inavyochajiwa. UNDP wametengeneza vituo vya kuchaji magari ya umeme unatokana na nguvu za jua.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi EWURA, Prof. Mark Mwandosya akiingia kwenye gari inayotumia umeme katika Ofisi za UNDP Mlimwa C Dodoma. Anayetizama kulia, ni Mjumbe wa Bodi ya EWURA na Mwenyekiti wa Kamati ya Nishati ya Bodi hiyo Bw.Harun Masebu.