Watu saba wamefariki dunia papo hapo na wengine 14 kujeruhiwa kwa ajali iliyohusisha malori mawili, bajaji na bodaboda katika eneo la Mpakani lililopo Tunduma wilayani Momba mkoani Songwe.
Akizungumza kwa njia ya simu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe, Theopista Mallya amekiri kutokea kwa ajali hiyo majira ya mchana wa Jana Julai 5, 2023, ambapo amesema wote waliofariki ni wanaume.
Kamanda Mallya amesema ajali hiyo imehusisha lori moja la IT, bajaji, bodaboda na lori lingine ambalo limepata hitilafu kwenye mfumo wa breki na kuyaparamia magari mengine.
Kamanda Mallya amesema majeruhi wamepelekwa katika Hospitali ya Mpakani Tunduma Wilayani Momba.
Cc; Eatv