Akiba Commercial Bank Plc inaendelea kujikita katika kuleta mapinduzi ya huduma bora za kibenki hapa nchini kwa kuendelea kuboresha huduma zake, hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Akiba Commercial Bank Plc, ndugu Silvest Arumasi wakati akiongea na waandishi wa habari katika banda la benki hiyo lililopo ndani ya viwanja vya sabasaba.
Mkurugenzi Mtendaji amesema kwamba; benki ya Akiba imeboresha huduma mbalimbali za kibenki ambazo zitaweza kukidhi matarajio ya wateja waliopo pamoja na wateja watarajiwa katika kujipatia huduma. Maboresho makubwa yamefanywa kwa huduma za wateja binafsi,(Personal banking) ambayo inawalenga Waajiriwa wa sekta za Umma na sekta binafsi ambapo mteja anaweza kupata mikopo ya aina mbali mbali kuendana na mahitaji yao mathalan, huduma za mikopo ya kujenga na kuboresha makazi, pia mikopo ya muda mfupi (Salary advance) kwa ajili ya kutatua dharura za kifedha kwa muda mfupi. Pamoja na hayo Benki imezidi kuboresha huduma za mikopo kwa wateja wakubwa (Corporate customers) kuendana na mahitaji ya soko. Vilevile, benki inatoa huduma za bima kwa wajasiriamali pamoja na vikundi mbalimbali ikiwemo mikopo ya bima –IPF (Insurance Premium Financing).
Aidha, Mkurugenzi ameendelea kusema kuwa benki imeboresha huduma za kibenki kwa kupitia Wakala (Akiba Wakala) na simu ya mkononi (Akiba Mobile).
Pamoja na hayo, benki imeboresha mifumo ya utumaji pesa kwenda nje ya nchi hivyo ametoa rai kwa wafanyabiashara kuchangamkia fursa hii. Amehitimisha kwa kuwashukuru wateja wote na kuwasisitiza waendelee kupata huduma bora za ACB na kuwaalika wajasiriamali pamoja na Wafanyakazi hapa nchini kuja kubenki na ACB ambayo ni benki sahihi na bora inayolenga kutimiza malengo ya Wateja wake.