Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini, TFF limeujuza umma kwamba Klabu Mbili ambazo ni Kitayosce iliyoko Ligi Kuu ya NBC na Fountain Gate inayocheza Ligi ya Championship zimefungiwa kufuatia kutofuata taratibu za kuvunja mkataba na aliyewahi kuwa Kocha ndani ya klabu hizo kwa vyakati tofauti.
Uamuzi huo umefanya na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) baada ya Kocha Ahmed El Faramawy Yousef Mostafa Soliman kushinda kesi ya Madai dhidi ya Klabu hizo.
Kocha huyo raia wa Misri ambaye ameshinda kesi, Klabu hizo zitatakiwa ziwe zimemlipa ndani ya siku 45 tangu uamuzi huo ulipotolewa lakini hazikutelekeza hukumu hizo.
Wakati FIFA imefungia Klabu hizo kufanya Uhamisho wa Wachezaji Kimataifa, TFF pia imezifungia Kufanya Usajili wa wachezaji wa ndani.
Hivyo, TFF imezikumbusha klabu kuzingatia mikataba inayoingia na Wachezaji pamoja na Makocha ili kuepuka adhabu mbalimbali ikiwemo kufungiwa usajili.
Aidha imezitaka Klabu kama zikitaka kuvunja mikataba na wachezaji au Makocha zinatakiwa kufanya kwa kuzingatia utaratibu.