Mshambulizi wa zamani wa Liverpool Roberto Firmino amesajiliwa na Al-Ahli ya Saudi Arabia baada ya mkataba wake wa kuitumikia klabu hio kumalizika.
Mbrazil huyo anajiunga kama mchezaji huru, akisaini mkataba wa miaka mitatu hadi 2026.
Firmino anaungana na mlinda lango wa zamani wa Chelsea aliyejiunga na Al-Ahli wiki moja iliyopita.
Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp alitaka kumbakisha mkongwe huyo, lakini Firmino alikataa kuingia kwenye mazungumzo ya mkataba mpya.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 alifunga mabao 111 katika michezo 362 akiwa na Liverpool baada ya kuwasili kutoka Hoffenheim mwaka 2015.