Klabu ya Pyramids FC ya Misri imemtambulisha rasmi mshambuliaji kutoka Congo Fiston Mayele akitokea kwa mabingwa watetezi wa Kombe la Ligi kuu ya NBC Tanzania, Young Africans Sports Club inayofahamika zaid kama Yanga. Hakika atakumbukwa sana Tanzania.
Mayele ameondoka Yanga ikiwa katika msimu mzuri kufuatia kuiwezesha klabu hio kutwa Ubingwa mara 2 mfululizo na kuweza kushiriki katika Fainali ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika, CAF.
Nyota huyo alifanikisha kupata tuzo mbalimbali zilizodhihirisha ubora wa kiwango chake awpo uwanjani.
Pyramids watakuwa wakicheza Ligi ya Mabingwa ya CAF kwa mara ya kwanza katika historia.
#KonceptTvUpdates