Dkt. Tulia ameyasema hayo Ijumaa Julai 15, 2023 wakati wa mkutano wa hadhara alioufanya katika Kata ya Iyunga Jijini humo kwa lengo la kuwajuza Wananchi baadhi ya ahadi alizozitekeleza katika Jimbo hilo ikiwemo Kata hiyo pamoja na yale yaliyofanywa na Serikali ya awamu hii.
“Niwaombe sana, watu hawa wapuuzwe na niwahakikishie tupo salama na hakuna cha bandari wala nchi inayouzwa na hata wakija hao wanaosema imeuzwa waambieni wawapatie mgao wa hayo mauzo” Amewekea mkazo Dkt. Tulia.
#KoncepttvUpdates