Klabu ya Yanga yazindua rasmi Jezi zake mpya zitakazotumika msimu ujao wa Soka Tanzania Bara 2023/2024.
Imezundua Jezi hizo kupitia mwaliko maalum nchini Malawi mbele ya Rais Lazarus Chakwera na Rais Dk. Samia Suluhu ambaye ndiye mgeni Rasmi kwenye sherehe za kuadhimisha mwaka mwingine toka nchini hio kujipatia uhuru wake.
Rais wa Klabu ya Yanga akiwa ktika Ikulu ya Rais wa Nchi hio aliwakabidhi Marais hao wawili Jezi mpya za klabu hio kuashiria uzinduzi rasmi wa Jezi hizo kuanza kutumika kwaajili ya msimu ujao wa michuano ya soka.
Muda mchache kupitia kurasa zqa mitandao ya kijamii za klabu hio ikataja wasambazaji na maduka rasmi ya kuweza pata jezi hizo ikitaja Maduka yote ya GSM nchi nzima na VunjaBei.
Yanga ndio klabu kubwa pekee iliyoanza kuzindua jezi zake mapema kabisa.