
Hatimaye mrimbwende Tracy Nabukera ameshinda Taji la Miss Tanzania Kwa toleo jipya la 2023/2024 na kukabidhiwa Gari aina ya Mercedes Benzi na kiasi cha Shilingi Milioni 10 kama zawadi Kwa mshindi pekee wa kwanza huku mshindi wa Pili akipewa Kiasi cha Shilingi Milioni 5.
Tracy amekabidhiwa taji la Umiss Tanzania na Halima Kopwe aliyekuwa miss Tanzania 2022-2023 ambapo Mgeni rasmi katika tukio hilo alikuwa ni Waziri mwenye dhamana ya Sanaa, Utamaduni na Michezo Mh. Pindi Chana akiwa na Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa Nchini (BASATA).