Mwanamume mmoja huko Mumbai nchini India, anayejulikana kama ‘mwombaji “Ombaomba” tajiri zaidi duniani,’ ametajwa kuwa na makadirio ya utajiri wake wa zaidi ya dola milioni moja!
Bharat Jain, ambaye hutumia siku zake akiomba pesa mitaani, Mali zake ni pamoja na nyumba kubwa ya yenye sehemu mbili 2, na pia huko Mumbai ana maduka mawili ya kukodi, hio humletea mapato ya kila mwezi kutoka rupi 60,000 hadi 75,000, au karibia $800.
Licha ya ushauri wa familia yake kuacha kuombaomba, Jain anaendelea kuomba mara kwa mara huku watoto wake wakiwa wamemaliza masomo yao na kupata ajira.