Beki mahiri wa Kandanda kutokea nchini Kenya Joash Onyango (30) amejiunga na Singida Fountain Gate kwa mkataba wa miaka miwili akitokea kwa Wanalunyasi Simba SC baada ya pande zote kukubaliana kuihama klabu hiyo.
Onyango anatoka Simba bila kikwazo chochote baada ya kuitumikia klabu ya Simba SC kwa misimu mitatu.
Hakuna nafasi ya kujiunga na Gor Mahia kama ilivyokuwepo na tetesi nyingi zikiripotiwa hio ni kufuatia kutowepo uthibitisho wowote naoonyesha kuna wigo wa mchezaji huyo kurejea tena katika Ligi ya Kenya.