Klabu ya Yanga imemtambulisha Mchezaji wa Zamani wa Simba Jonasi Mkude “NUNGUNUNGU” ambaye alimaliza mkataba wake kuhudumu ndani ya Klabu hio.
Mkude amejiunga na Yanga akiwa mchezaji huru baada ya kuitumikia Klabu yake ya zamani kwa misimu Zaidi ya 10.
Yanga imemfanyia utambulisho mkubwa na wa kipekee kwa kuzingatia heshima aliyonayo Mchezaji huyo katika historia ya Mpira wa hapa nchini