Jenerali Abdourahamane Tchiani ndiye kiongozi mpya wa Niger kufuatia mapinduzi ya kijeshi, kama televisheni ya taifa ilivyoripotiwa Ijumaa, siku mbili baada ya Rais wa nchi hiyo Mohamed Bazoum kuzuiliwa na walinzi wake.
Akionekana kwenye televisheni ya taifa, jenerali huyo alisema wanajeshi wametwaa mamlaka kutokana na kuzorota kwa hali ya usalama katika nchi hiyo ya Sahel.
Jenerali huyo alisema kwamba wakati Rais mteule wa Niger Mohamed Bazoum alijaribu kuwashawishi watu kwamba “yote yanakwenda sawa … hali imezidi kuwa mbaya, rundo la watu, waliokimbia makazi yao, unyonge na kufadhaika”.
Cc; France 24
#KonceptTvUpdates