Mmiliki wa mtandao wa Twitter, Elon Musk @elonmusk amesema wanapanga kubadilisha nembo ya Mtandao huo kutoka kwenye ndege wa bluu, kuwa herufi ‘X’, kuashiria mageuzi makubwa yaliyofanyika tangu alipoununua mtandao huo. . Ikumbukwe kuwa Bilionea huyo anayemiliki makampuni mbalimbali ikiwemo SpaceX, mnamo oktoba 2022, alituma ujumbe kupitia Twitter, kuwa kununua mtandao huo ni kuongeza kasi ya kuunda ‘X’. . Musk ametajwa kuwa na historia ndefu na herufi hiyo, kwani mnamo mwaka 1999 alianzisha kampuni ya huduma za kifedha iliyojulikana X.com, ambayo kwa sasa inajulikana kama PayPal.