Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetangaza bei mpya kikomo za bidhaa za mafuta ya petroli nchini zinazoanza kutumika leo Julai 5, 2023.
Katika bei hizo, mafuta ya petroli na dizeli yaliyopokelewa bandari ya Dar es Salaam zimeshuka kwa shilingi 137 kwa lita na 118 kwa lita.
Kwa mikoa ya Kaskazini, bei ya rejareja ya mafuta ya petroli imeshuka kwa shilingi 188 kwa lita wakati bei ya dizeli imeongezeka kwa shilingi 58 kwa lita. Kwa mikoa ya Kusini, hakuna shehena ya bidhaa ya mafuta iliyopokelewa bandari ya Mtwara, hivyo bei zitaendelea kuwa kama ilivyotangazwa Juni, 2023.
“BEI KIKOMO ZA MAFUTA AINA YA PETROLI ZITAKAZOANZA KUTUMIKA KUANZIA JUMATANO TAREHE 5 JULAI 2023.” Ewura