ADVERTISEMENT
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
Saturday, September 23, 2023
  • Login
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
No Result
View All Result

MBUNGE WA MBARALI AFARIKI AJALI YA PIKIPIKI

Mbeya

MTEWELE ALFRED by MTEWELE ALFRED
Jul 2, 2023
in HABARI
0
MBUNGE WA MBARALI AFARIKI AJALI YA PIKIPIKI
0
SHARES
141
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

RelatedPosts

KADHIA YA MAJI KUTUAMA DAR ES SALAAM: MBUNGE MALECELA AHOJI KAULI YA SERIKALI

KADHIA YA MAJI KUTUAMA DAR ES SALAAM: MBUNGE MALECELA AHOJI KAULI YA SERIKALI

Aug 29, 2023

MCHANGO WA MIKOPO YA ELIMU KWA WANAFUNZI WA SHULE BINAFSI NCHINI TANZANIA

Aug 29, 2023

WAZIRI AWESO AZINDUA MRADI WA MAJI KALIUA, TABORA

Aug 1, 2023
Load More

Mbunge wa Mbarali afariki ajali ya pikipiki | East Africa TelevisionMbunge wa Jimbo Mbarali mkoani Mbeya Francis Mtega amefariki dunia kwa ajali baada ya pikipiki aliyokuwa akisafiria kutoka shambani kurejea nyumbani kugongana na ‘Powertilla’ katika Tarafa ya Ilongo Kata ya Chimala.

Akizungumza na Mwananchi Jana Julai Mosi, Mkuu wa Wilaya (DC) ya Mbarali, Kanali mstaafu Denis Mwila amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo leo Julai Mosi 2023 saa 9 alasiri baada ya pikipiki aina ya Boxer yenye namba za usajili MC 573 CGY aliyokuwa akiendesha marehemu kugangana na ‘Powertilla.’

Amesema ajali hiyo imetokea kwenye barabara ya vumbi wakati marehemu akitokea shambani kwake akielekea Kata ya Chimala wilayani Mbarali ambako alikuwa akiishi.

“Tayari dereva wa ‘Powertilla’ Alex Musa (18) anashikiliwa na Polisi na chanzo cha ajali ni uzembe wa dereva huyo ambaye hakuchukua tahadhari na kuendelea mwendo mbaya kwenye barabara ya vumbi jambo ambalo lilisababisha ajali hiyo,” amesema Kanali Mwila na kuongeza;

“Tulishatoa tahadhari na masharti madereva wote wa ‘Powertilla’ ifikapo saa 12 jioni kutofanya kazi kutokana na madereva wake kutokuwa na leseni, lakini pia nyingi hazina taa zinazoweza kuonyesha usalama wawapo barabarani,” amesema.

Awali, wakati akitangaza kifo hicho, Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson ametoa pole kwa familia ya marehemu, ndugu, jamaa, wabunge na wananchi wa Jimbo la Mbarali.

“Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Mheshimiwa Francis Leonard Mtega. Natoa pole kwa familia ya Marehemu, ndugu, jamaa, Waheshimiwa Wabunge na Wananchi wa Jimbo la Mbarali. Mwenyezi Mungu awape moyo wa uvumilivu na subira katika kipindi hiki kigumu,” amesema Spika Tulia.

Taarifa kutoka Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Kimataifa cha Bunge imesema kuwa Ofisi ya Bunge kwa kushirikiana na familia ya Marehemu inaratibu mipango ya maziko na taarifa zaidi zitaendelea kutolewa.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa Wabunge Mkoa wa Mbeya, Oran Njeza amesema kuwa amepokea taarifa za kifo cha Mbunge huyo na kwa sasa yuko njiani kurejea Mbeya akitokea Dodoma.

“Ni kweli nimepokea taarifa za kifo chake bado tunaendelea kufuatilia kwani kwa sasa nipo njiani natokea Dodoma kurejea Mbeya,” amesema.

Naye Mbunge wa Lupa Wilaya ya Chunya, Masache Kasaka amesema wamepokea taarifa za kifo hicho kwa mshtuko mkubwa kwani hivi karibuni walikuwa naye kwenye vikao vya Bunge mjini Dodoma.

“Tumempoteza mtu muhimu sana alikuwa na ushirikiano mkubwa na wabunge wenzake na kwamba wamepokea taarifa hizo kwa mshtuko mkubwa sana,” amesema.

Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake (UWT) Wilaya ya Mbarali, Zabibu Nuroo amesema kama chama wamepokea taarifa hizo kwa mshtuko mkubwa na kwamba wamepoteza mtu muhimu aliyekuwa akiwaunga mkono kwa hali na mali

“Kimsingi binafsi nimepata pigo kubwa sana kutokana na juhudi zake kuunga mkono shughuli za chama kwa sasa tunasubiri taratibu za kifamilia ili kujua maziko taratibu za maziko,” amesema.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Benjamin Kuzaga amesema kwa sasa yuko njiani anaelekea Wilaya ya Mbarali na atatoa taarifa kamili mara baada ya kufika eneo la tukio.

Cc; Mwananchi

Related

Tags: BUNGE LA TANZANIAIKULU MAWASILIANOMBARALI
MTEWELE ALFRED

MTEWELE ALFRED

Related Posts

Maurel and Prom: Empowering Tanzania’s Sustainable Energy Economy
BIASHARA

Maurel and Prom: Empowering Tanzania’s Sustainable Energy Economy

by I am Krantz
Sep 22, 2023
DR KONGO YATAKA MONUSCO KUONDOKA HARAKA
HABARI

DR KONGO YATAKA MONUSCO KUONDOKA HARAKA

by SUZO SHUKRANI
Sep 21, 2023
HAIER TANZANIA NA AZAM TV WAUNGANA KUKIWASHA KWA PAMOJA
HABARI

HAIER TANZANIA NA AZAM TV WAUNGANA KUKIWASHA KWA PAMOJA

by SUZO SHUKRANI
Sep 21, 2023
MNH YAFANYA UPASUAJI WA KWANZA TUNDU DOGO MOJA
AFYA

MNH YAFANYA UPASUAJI WA KWANZA TUNDU DOGO MOJA

by SUZO SHUKRANI
Sep 21, 2023
SBL KUUNGANISHA TAMADUNI KUPITIA OKTOBA FEST
HABARI

SBL KUUNGANISHA TAMADUNI KUPITIA OKTOBA FEST

by SUZO SHUKRANI
Sep 21, 2023
TAWA YATAKIWA KUJIPANGA KUONGEZA UKUSANYAJI MAPATO
HABARI

TAWA YATAKIWA KUJIPANGA KUONGEZA UKUSANYAJI MAPATO

by SUZO SHUKRANI
Sep 21, 2023

KRANTZ MWANTEPELE (FOUNDER & CEO)

KONCEPT TV

https://www.youtube.com/watch?v=0HP0mB_rtIU&t=7s
KONCEPT TV

KONCEPT TWEETS

July 2023
M T W T F S S
 12
3456789
10111213141516
17181920212223
24252627282930
31  
« Jun   Aug »
Currently Playing
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In