Mh. Ummy Mwalimu katika ukurasa wake wa twitter amesema “Ni heshma kubwa kukutana na kufanya mazungumzo na Dkt. Ravindrapath Kancharla, Mwenyekiti Mwanzilishi wa Global Health Foundation ya Hayderabad.”
“Taasisi hii imejipanga kuleta mapinduzi katika sekta ya Afya duniani kwa kuleta pamoja Mafunzo kwa Wataalam wa Afya, Sayansi, Huduma za Afya, Tehama na Ubunifu. Hivi sasa wameshatengeneza program ya mafunzo ya mtandaoni ya kuwezesha watoto wenye usonji (Autism) kuongea/kuwasiliana na pia kujihudumia”.
Aidha wametengeneza program ya kufuatilia ubora wa huduma kwa watu wanaosafisha damu (dialysis). Tanzania tutanufaika na ubunifu huu.
#@ummymwalimu
#@KonceptTvUpdates