Mnamo julai 5 Mwaka huu Mtandao mpya wa Threads chini ya kampuni ya Meta ulizinduliwa rasmi na huku ukitajwa kuwa ni mtandao ulioanzishwa kuweza shindanishwa na Mtandao mwingine wa toka hapo zamani Twitter, kwa hapo mwanzo uliteka mamilioni ya watumiaji wapya kuanza lakini baadae imeonekana kushuka katika matumizi yake kwa utofauti mkubwa.
Kwa mujibu wa Jarida la Forbes linaloangazia masuala ya masoko, teknolojia na mawasiliano, limesema mtandao mpya wa Threads umepungua matumizi ya watumiaji wake (Engagement) kwa karibu asilimia 70.
Mtandao mpya wa threads umepungua matumizi ya watumiaji wake (Engagement) kwa karibu asilimia 70, jarida la Forbes limebainisha.
Watumiaji wa kila siku wa Threads ni takriban milioni 13 chini kutoka milioni 44 mnamo Julai 7 na wastani wa muda unaotumika kila siku kwenye mtandao huo mpya ni dakika nne, ambayo ni chini kutoka kwa kilele chake cha siku ya uzinduzi cha dakika 19, kulingana na Sensor Tower.
Haya yanajiri baada ya kampuni hiyo kuripoti kuwa ilisajili watu milioni 100 ndani ya wiki moja baada ya kuzinduliwa mnamo Julai 5.
Twitter ina takriban watumiaji milioni 200 wanaotumia kila siku na wastani wa muda unaotumika kila siku kwenye jukwaa ni dakika 30, kulingana na Sensor Tower.
Kwa mtazamo wako wewe unaona wamiliki wa mtandao huo wamekwama wapi hadi kupelekea kutokea kwa changamoto hio?
Cc; Forbes
#Mwananchi
#KoncepttvUpdates