Klabu ya As Far Rabat ya nchini Morocco imeingia mkataba wa Makubaliano na Kocha wa Zamani wa Yanga SC Nasreddine Nabi kuwa Kocha mpya kwa dili la miaka miwili ndani ya klabu hio.
Nabi anakaimu nafasi hio na Baada ya Kocha mkuu wa Timu hio kuondoka.
Hapo awali Kocha huyo alitazamiwa zaidi kujiunga na klabu ya Kaizer Chiefs ile baada tu ya kuachana na Yanga lakini mambo yakaonekana kwewnda kombo kuweza fikia makubaliano baina yao, na hivi karibuni ndio ameweza kujiunga na familia hio ya AS FAR RABAT.
Anaonesha amekubali yale yaliopita akitazamia zaidi kupata changamoto mpya akiwa na timu nyingine.
Nabi ameondoka nchini Tanzania akiicha Klabu ya Yanga ikiwa katika kilele kikubwa cha mafanikio hio ni kufuatia kuiwezesha klabu hio kutwaa mataji mengi mfululizo hasa msimu wa mwisho amefanikishia kukusanya makombe yote ya Michuano ya Soka Tanzania Bara akianzia na Ngao ya Hisani (Jamii), Kombe la Shirikisho la AZAM SPORTS na Ligi kuu ya NBC ikiambatana na kucheza Fainali za Kombe la Shirikisho Barani Afrika (CAF Confedaration Cup).
#KonceptTvUpdates