Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule akipokea jezi ya NBC Dodoma Marathon 2023 kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi ikiwa ni maandalizi ya kushiriki mbio za mwaka huu zitakazofanyika Jumapili, Julai 23. Wanaoshuhudia kushoto ni Hapiness Kizigira kutoka NBC na wa kwanza kulia ni DAS wa wilaya ya Dodoma Sakina Mbugi akifuatiwa na mkuu wa wilaya ya Dodoma Jabir Shekimweri.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule (kulia) pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi wakionyesha jezi za kukimbilia muda mfupi baada ya kutangaza kukamilika kwa maandalizi yam bio za NBC Dodoma Marathon 2023 zitakazofanyika Jumapili, Julai 23. Mbio hizo zinalenga kukusanya shilingi milioni 500 kwa ajilya kusaidia mapambano dhidi ya kansa ya shingo ya kizazi nan a kusomesha wakunga ili kupunguza vifo vinavyotokana na uzazi.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule (katikati) akionyesha jezi zitakazotumika katika mbio za NBC Dodoma Marathon 2023 akiwa na mkurugenzi mtendaji wa NBC Theobald Sabi pamoja na viongozi wa mkoa wa Dodoma ikiwamo Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Jabir Shekimweri. Mbio hizo zinalenga kukusanya shilingi milioni 500 kwa ajilya kusaidia mapambano dhidi ya kansa ya shingo ya kizazi nan a kusomesha wakunga ili kupunguza vifo vinavyotokana