Klabu ya Simba imefanikisha zoezi lake la kuzindua Jezi zake za kutumika msimu ujao 2023/2024 juu ya kilele cha Mlima Kilimanjaro kama ilivyotangazwa kufanyika hivyo wiki moja iliyopita.
Kwa msimu huu Simba imetambulisha jezi zake mpya ikiwa imeingia mkataba mpya wa miaka miwili na kampuni ya Sandaland ambayo inakuwa ndio mzalishaji na msambazaji rasmi wa jezi zake.
Kabla ya kampuni hio Simba ilikuwa na kampuni ya VunjaBei katika nafasi hio ya Uzalishaji na Usambazaji wa Jezi ambayo imemaliza mkataba wake smimu uliopita.
#KoncepttvUpdates
Mashujaa hawa hapa Wametimiza lengo la klabu ya Simba kuzindua jezi kwenye kilele cha Mlima Kilimanjaro. Hivyo watajwa kustahili kutambuliwa kwa kazi kubwa waliyofanya ambapo katika siku ya #SimbaDay2023 wanatarajiwa kutunukiwa vyeti maalum.
#KoncepttvUpdates