Kiongozi wa chama cha muungano cha Azimio la Umoja One Kenya Raila Odinga, ambaye amezua wasiwasi baada ya vuta nikuvute wakati wa maandamano yanayoendelea dhidi ya serikali, sasa anasema anapata nafuu kutokana na homa ya mafua.
Odinga, ambaye hakufichua aliko kwa sasa, anasema alikuwa mgonjwa kidogo, na hivyo kuweka swali la kwa nini amekosekana uwanjani tangu maandamano ya siku tatu yalipoanza Jumatano lisalie bila jibu kamili.
Cc; CitizetvKenya
#KoncepttvUpdates