Kufuatia kutungwa kwa Sheria ya Mipango ya Taifa ya Mwaka 2023 pamoja na uamuzi wa kuhamishia masuala ya uwekezaji Ofisi ya Rais, hivyo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya mabadiliko madogo ya Miundo ya Wizara na kufanya uteuzi wa viongozi.
Rais Dkt. Samia Suluhu @SuluhuSamia ameunda Wizara ya Fedha ambapo amemteua Mwigulu Nchemba @mwigulunchemba1 kuwa Waziri wa Fedha. Kabla ya uteuzi huo alikuwa ni Waziri wa Fedha na Mipango.
Profesa Kitila Mkumbo, ameteuliwa kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji
Ameunda Wizara ya Viwanda na Biashara ambapo amemteua Dkt. Ashatu Kachwamba Kijaji kuwa Waziri wa wizara hiyo. Kabla ya uteuzi huo alikuwa Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara.
amemteua Lawrence Nyasebwa Mafuru kuwa Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango ya Taifa. Kabla ya uteuzi huo alikuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha na Mipango (Usimamizi wa Uchumi).
Amemteua Elijah Mwandumbya kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha (Usimamizi wa Uchumi). Kabla ya uteuzi huo alikuwa Kamishna, Idara ya Uchambuzi wa Sera, Wizara ya Fedha na Mipango.