Katika ukurasa wake wa Twitter jana saa nne usiku, Rais wa Uganda Yoweri K. Museveni amesema, amepokea ujumbe kutoka Ubeligiji. Alisema “Ujumbe kutoka Bridgin Foundation ukiongozwa na Rais wao, Prof Tanko Mouhamadou na H.E Mirjam Blaak, Balozi wetu nchini Ubelgiji wamenitembelea Entebbe leo”.
“Nilielezwa kuhusu maendeleo ya ujenzi wa hospitali ya kufundishia nchini Uganda na uanzishwaji wa Makao Makuu ya Sekretarieti ya Jukwaa la Vyuo Vikuu vya Mkoa la Kujenga Uwezo katika Kilimo (RUFORUM), pamoja na kituo cha mikutano na Hoteli”.
Alisisitiza kuwa mpango huo ni fomula ya ushindi na Afrika ambao wamekuwa wakiunga mkono nchi za Magharibi hata kabla ya uhuru kwa uwezo wetu wa kununua.
Aidha, Uganda kutokana na mpango huo, iutakuwa na ustawi mkubwa wa kimataifa ikiwa makampuni kutoka nchi za Magharibi yatapenda kuwekeza barani Afrika hasa katika bidhaa zilizomalizika badala ya kulenga kuagiza malighafi kutoka nje.
Nchi nyingi barani Afrika zimekuwa zikitegemea bidhaa zilizokamilika kutoka nchi za magharibi na mashariki ya mbali, hii ni kutokana na uwepo wa uwezo mdogo wa kisayansi, teknolojia na maendeleo kiujumla ukilinganisha na nchi za magharibi.
#@Yowerikaguta
#KonceptTvUpdates