Ushindani unaojitokeza kati ya Wasanii wa HipHop wa nani anayeweza miliki vito vya thamani zaidi unatokea maeneo mengi na hivyo kupelekea wasanii hao kuishi kwa gharama kubwa.
Rapa kutokea kipande cha nchini Marekani Rick Ross (William Leonard Roberts II) hapo jana alidhihirisha umiliki wake wa hivi punde wa kupindukia kwenye Instagram— akionyesha Saa ya mkononi ya kipekee yenye thamani ya dola Milioni 20! (ambayo ni sawa na Bilioni Nne na Milioni Mia Nane na Sabini/ TZS. 48,700,000,000)
Saa, iliyoundwa na Jacob The Jeweler, ambayo ilichukua zaidi ya miaka mitatu kukamilika, ikiwa imepambwa kwa mamia ya vito vya thamani. Wakati watu wengine mashuhuri wamewahi kuonyesha saa zao za kifahari, saa ya Ross inaweka rekodi mpya katika suala la bei na adimu, hivyo kuwazidi wengine!
Wadau wengi wametoa maoni yao kuhusu ununuzi wa Saa hio,Baadhi waonekana wakimsifu kwa umiliki wa saa hio ya Gharama huku wengine wakikosoa vikali kuwa ni mbaya kwa muonekano na ni matumizi mabaya ya pesa.