Nyota wa Kimataifa wa Mpira wa Miguu kutokea nchini Tanzania Mbwana Ally Samatta aliyekuwa anakipiga mnamo klabu ya Genk rasmi amejiunga na Klabu ya PAOK FC inayoshiriki Ligi kuu ya Ugiriki.
Atambulishwa mtandaoni, amejiunga na Klabu hio akiwa mchezaji huru akitokea klabu ya Genk ya Ubelgiji
Samatta kwa sasa alishakuwa mzoefu zaidi katika Soka la nchini Ubelgiji kutokana ameweza shiriki Michuano Mingi ndani ya Ligi ya nchini humo katika misimu tofauti.
Ikumbukwe kuwa Samatta alianza kuichezea Genk kabla ya kwenda Fenerbahce na kisha akarejea tena ndani ya kikosi cha Genk baada ya muda fulani na hivi karibuni ndio ametambulishwa ndani ya wakali hao wa Soka kutokea Ugiriki.