Simba Sports Club imeweka wazi viingilio vyote kwa siku ya simba day inayotarajiwa kufanyika siku ya tarehe 6 ya mwezi Agost.
viingilio hivyo ni Platinum – Tsh. 200,000, VIP A – Tsh. 40,000, VIP B – Tsh. 30,000, VIP C – Tsh. 20,000, Machungwa – Tsh. 10,000 na Mzunguko – Tsh. 5,000
Aidha kwa upande wake msemaji wa timu hiyo Ahmed Ally amesema “Sisi kama klabu tunahitaji fedha lakini kwenye tamasha tunahitaji zaidi mashsbiki, wanasimba waje na jezi zaidi ndiyo maana tunawatafuta wadhamini kama CRDB ili walete fedha. Tunajali zaidi maslahi ya Wanasimba”.
Simba day ambayo itatanguliwa na uzinduzi wa simba week siku ya tarehe 29, julai 2023, ambayo pia itaambatana na mtaukioa kadhaa kama vile kuchangia damu, shughuli mbalimbali za kijamii ikiwa ni pamoja na kufanya usafi hospitali, masoko pamoja na uwepo wa siku maalum ya kutembelea mashujaa wa simba.
pia, katika siku hiyo kutakuwa na wasanii mbalimbali ambao wataipamba siku hiyo wa kutumbuiza na nyimbo mbalimbali. Miongoni mwa wasanii watakao shiriki ni Tundaman, Meja Kunta na Whozu.
#simbasctanzania
#KonceptTvUpdates