Klabu ya Simba imetangaza rasmi siku maalum ambazo matukio mawili muhimu yakihusisha Uzinduzi wa Jezi mpya kwa ajili ya msimu ujao 2023/24 na kufanyika kwa Tamasha la Simba Day yataweza chukua nafasi ndani ya klabu hio.
Jezi mpya zinatarajiwa kuzinduliwa rasmi Julai 21 juu ya Mlima Kilimanjaro kwenye kilele cha Uhuru muda wa Saa 1:00 Usiku itakuwa Mubashara kutoka Mlima huo Mrefu Barani Afrika.
Klabu hio imekuja na wazo la kipekee na la kihistoria kwani moja itatangaza uwepo wa Vivutio vya Utalii vilivyopo nchini Tanzania na pia, itaongeza chachu ya Wageni wengi kutembelea nchi na Pato la Nchi kupitia Sekta ya Utalii na Maliasili kuongezeka maradufu
Aidha Msemaji wa Simba SC Ahmed Ally ametolea ameeleza kuwa sababu ya kurudisha nyuma siku ya Simba Day kutoka Tarehe Agosti 8 hadi imekuwa Agosti 6 ni kuwa inataka kuwapa nafasi wachezaji wa klabu hio kupata muda mzuri wa kupumzika kabla ya Mechi ya kwanza dhidi ya Singida Fountain Gate FC katika kuwania Ngao ya Hisani (Jamii).
“Ijumaa saa 1:00 usiku jezi itakuwa imefika kileleni kwenye Mlima Kilimanjaro. Itazinduliwa na itaonekana rasmi siku hiyo.”- CEO Imani Kajula.
“Jezi zetu zitazinduliwa July 21 2023 Juu ya Mlima Kilimanjaro kwenye Kilele cha Uhuru saa 1:00 Usiku tukio litakua Live kutoka Mlimani” Amesisitisa Ahmed Ally
“Simba Day itakuwa Agosti 6, tumeirudisha nyuma siku mbili sababu Agosti 10 tutakuwa na mchezo wa Ngao ya Jamii hivyo tunataka wachezaji wetu wapate muda wa kupumzika,” Ahmed Ally, Meneja Habari na Mawasiliano Simba SC
#KoncepttvUpdates