Klabu ya Simba SC (@simbasctanzania) imemtambulisha beki mahiri Che Malone Fondoh kutoka klabu ya Conto Sport FC inayoshiriki Ligi ya MTN Elite One ya nchini Cameroon kwa mkataba wa miaka miwili.
Malone alikuwa nahodha wa Coton Sport ambayo ilinyakua ubingwa msimu uliopita 2022/23 nchini humo huku yeye akiibuka mchezaji bora wa Ligi hiyo.
Mchezaji huyu anakuwa wa 3 katika Utambulisho wa Sajili mpya kwenye kikosi cha Simba SC kupitia Dirisha kubwa kuelekea michuano ya Msimu ujao.
#KoncepttvUpdates