
Simba SC imethibitisha kuwa imefikia makubaliano na klabu ya Quevilly Rouen Metropole (QRM) ya nchini Ufaransa kumnunua mchezaji wao Pape Sakho.
Aidha Simba SC imemtakia kila la kheri Sakho kwenye timu yake mpya.
Msenegal huyo ni moja ya wachezaji machachari na mwenye uwezo wa kukimbia na mpira kwa uharaka afikapo katika eneo la kusogeza mashambulizi kwenye lango la timu pinzani hivyo ameweza kusaidia kikosi ya Simba kuwa bora kwa msimu alipokuwa akiitumikia.
Sakho atakumbukwa pia kutokana na aina yake ya Ushangiliaji pale anapofanikisha kuuweka mpira nyavuni unaofahamika kama “Kunyunyiza”
Alikuwa miongoni mwa rafiki wa karibu sana na Mchezaji mwenzake Peter Banda hadi wakapeana majina ya utani “Tom and Jerry”
Japo klabu ya Simba imeweza achana na nyota huyo bado pande zote mbili zinayavyo vya kujivunia katika sehemu ya mafanikio yake kuanzia Ligi ya ndani na Michuano ya Soka ya Kimataifa ikijumisha Klabu Bingwa Barani Afrika.
#KonceptTvUpdates