kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia, watu wengi hulazimika kutumia simu, kompyuta na hata vishikwambi katika kuapata taarifa mbalimbali, kufanya biashara na mambo kadha wa kadha pia katika kuhakikisha wanaendana na kasi ya maendeleo hayo.
Rekodi zinaonyesha kati ya April hadi Juni 2023 dakika bilioni 34.81 zilitumika katika maongezi ya simu. Huku dakika 18,644,312 sawa na 53.4% ni za ndani ya Mtandao (On Net Calls) ambapo Airtel inaonoza kwa 40%, Vodacom 30%, Tigo 23%, Halotel 7%, TTCL 0.24% na Smile 0.00%
Simu za mtandao mmoja kwenda mtandao mwingine (Off Net Calls) zilikuwa 16,166,491,477 sawa na 46.4%. Mtandao wa Tigo ndiyo unaoongoza kwa 29%, Airtel 28%, Vodacom 26%, Halotel 16%, TTCL 1% na Smile 0.01%
Aidha TCRA imetoa lai kwa watumiaji wa simu kuwa “Iwapo utasafiri nje ya nchi na hautotumia laini yako kwa muda wa siku 90 mfululizo, toa taarifa kwa mtoa huduma wako ili kuepuka kufungiwa”
#tcra_tanzania
#jamiiforums
#Mawasiliano
#KonceptTvUpdates