Fabrice Ngoma si mchezaji tena wa Al Hilal SC, imethibitishwa. Kesi kutoka kwa klabu hio haitakuwa suala kwani FIFA tayari imetoa idhini lakini bado Hilal haijakata tamaa.
Yanga SC walikuwa wa kwanza kufanya mawasiliano na wakatoa fursa ya kumsajili Ngoma wiki kadhaa zilizopita kama ilivyoripotiwa. Mchezaji tayari alisema “ndio” lakini suala la marufuku kwenye TMS ya FIFA ilipelekea baadhi ya mambo yakabadilika. Simba SC walichangamkia fursai hiyo na kuipiku papo hapo.
Ngoma amepewa mkataba wa miaka miwili na sasa atacheza Simba. Wazo la kucheza Super League Afrika lilimvutia Ngoma. Fahamu: Ngoma anaweza akatangazwa kuwa mchezaji mpya wa Simba SC wiki hii na kuwa sehemu ya kikosi kitakachokwenda Uturuki wiki ijayo kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao. (Micky Jnr)
#Transfer
#Mpira wa Afrika