Mkurugenzi wa Miundombinu na Mtandao wa Vodacom Tanzania Plc Bw. Andrew Lupembe (kushoto) na Mkurugenzi wa TEHAMA Bw. Athumani Mlinga (kulia) wakipokea tunzo ya kampuni inayoongoza kwa teknolojia barani Afrika baada ya kuibuka kinara miongoni mwa makampuni ya Vodacom yaliyoko Afrika. Tunzo hii imekabidhiwa na Dejan Kastelic, Afisa Mkuu wa Teknolojia kutoka kundi la makampuni ya Vodacom wakati wa hafla iliyofanyika mwanzoni mwa wiki hii jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Idara ya Usalama Mtandaoni wa Vodacom Tanzania PLC, Joel Kazyoba (kulia) akipokea tunzo ya kampuni inayoongoza kwa teknolojia barani Afrika baada ya kuibuka kinara miongoni mwa makampuni ya Vodacom yaliyoko Afrika. Tunzo hii imekabidhiwa na Dejan Kastelic, Afisa Mkuu wa Teknolojia kutoka kundi la makampuni ya Vodacom wakati wa hafla iliyofanyika mwanzoni mwa wiki hii jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Idara ya Usalama Mtandaoni wa Vodacom Tanzania PLC, Joel Kazyoba (wa pili kulia) akipokea tunzo ya kampuni inayoongoza kwa teknolojia barani Afrika baada ya kuibuka kinara miongoni mwa makampuni ya Vodacom yaliyoko Afrika. Tunzo hii imekabidhiwa na Dejan Kastelic, Afisa Mkuu wa Teknolojia kutoka kundi la makampuni ya Vodacom wakati wa hafla iliyofanyika mwanzoni mwa wiki hii jijini Dar es Salaam. Wakifurahia tukio hilo kwa pamoja kushoto ni Mkurugenzi wa Miundombinu na Mtandao wa Vodacom Tanzania Plc Bw. Andrew Lupembe na kulia ni Mkurugenzi wa TEHAMA Bw. Athumani Mlinga.