Klabu ya Yanga imesthibitisha kukamilisha usajili wa Mchezaji Nickson Kibabage kutokea Singida Fontain Gate FC ambapo amehudumu kwa mara ya mwisho msimu uliopita ikiwa bado inafahamika kama Singida Big Stars kabla ya Kuuzwa rasmi.
Kibabage anajumuika rasmi na Wanajangwani hapa ni mwendo wa “Green and Yellow” ili kuweza kuitumikia klabu yake mpya kuanzia msimu ujao wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara.
Mchezaji huyo ni Chimbuko zuri kutoka Mtibwa Sugar U-17 na U-20, kulingana na uwezo aliouonyesha kwenye Michuano ya Ligi kuu ya Vijana U-20 kupitia timu hio ikampa nafasi ya kusajiliwa na Singida BS (Singida Fountain Gate).
Hatimaye kwa sasa amekuwa na wakati mzuri kutua katika miongoni mwa Timu kubwa iliyojaa Wadau na Mashabiki wengi hapa Nchini.