Muda mfupi baada ya kikundi cha kijeshi nchini Gabon kumuondoa madarakani rais wa nchi hiyo Ali Bongo kisha kumuweka kizuizini, rais huyo ameonekana katika video inayomwonyesha akituma ujumbe wa kuomba msaada kwa mataifa yote duniani ambayo anaamin ni marafiki zake.
katika video hiyo amesema “Mimi Ali Bongo Odimba, rais wa Gabon, ninatuma ujumbe kwa marafiki wote duniani kote kuwaambia wapige kelele kwasababu watu wamenikamata. Mtoto wangu yuko mahali kwingine, mke wangu yuko sehemu nyingine na mimi niko kwenye makazi yangu. Kwasasa niko kwenye makazi yangu na hakuna kinachoendelea sijui ni nini kinachoendelea. Hivyo, nawaita mpige kelele, mpige kelele kweli. Nawashukuru”.
Gabon kwa zaidi ya miaka 43 imekuwa ikiongozwa na ukoo mmoja wa Odimba, huku baba yake Ali Bongo akitajwa kuwa ni kiongozi ambaye ametajirika sana na kuishi maisha ya anasa katika kipindi chake cha uongozi, leo hii jarida a ukoo huo linafungwa na wanajeshi waliochukua madaraka kwa kumpidua Ali Bongo.
#KonceptTvUpdates