Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amemteua balozi Ali Idi Siwa kuwa mkurugenzi mkuu wa idara ya usalama wa taifa.
Balozi Siwa ameapishwa jana Agosti 28, 2023 ikulu jijini Dar es salaam na kuchukuwa nafasi ya Bw. Said Hussein Massoro ambaye ameteuliwa kuwa balozi.
Massoro aliteuliwa kushika nafasi hiyo Januari 3 mwaka huu na kudumu kwenye ofisi hiyo nyeti kwa miezi nane kabla ya kuteuliwa kuwa Balozi.
Kabla ya uteuzi huo Balozi Siwa alikuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) nafasi aliyohudumu tangu Septemba 20, 2018.
Kabla ya hapo alikuwa Balozi wa Tanzania nchini Rwanda kwa takribani miaka mitatu kuanzia 2015 hadi 2018.
#KonceptTVUpdates