Ikiwa zimesalia siku chache kufikia kilele cha tamasha la Simba Day, Klabu hio imeendeleza hamasa kwa mashabiki kwa namna yake, Simba SC imefanya maandamano yaliyoanzia roundabout Kwa Mama Kibonge kuelekea Buza Kanisani ambapo ndipo uzinduzi wa hamasa ya wiki ya Simba umefanyika.
Matukio mbalimbali yametokea lakini jambo la kuhusiana na Kibegi kingine cha “SHABIKI BINGWA” ndio kimewavutia mashabiki wengi kwa sababu wameachwa na shauku ya bkutaka kuju nini kilichowekwa ndani yake.
Meneja Habari na Mawasiliano SC Ahmed Ally amefunguka kuwa ndani ya siku ya kilele cha SIMBA DAY kutakuwa na matukio mengi sana hivyo awataka wadau na mashabiki wa klabu hiyo kununua tiketi bila kikomo ili wakaujaze uwanja.
Hapa chini ni baadhi ya matukio mengineyo yaliyojitokeza katika hafla hiyo;