Leo, mashabiki wa soka wanajitayarisha kwa mtanange mkubwa katika dimba la ABEBE BIKILA. Timu yenye kibendera cha taifa chetu kinachopepea kwa fahari, itapambana na Bahir Dar Kenema katika mzunguko wa kwanza wa CAF Confederation Cup. Mechi hii inatarajiwa kuwa na msisimko mkubwa na ushindani wa hali ya juu.
Azam Fc ikiwa imejiandaa kwa kushirikiana kwa bidii na kocha wao, na wachezaji kwa ujumla wao, wamejitolea kwa moyo wote ili kuleta ushindi. Bahir Dar Kenema pia wamekuwa na mazoezi makali, na hawatapunguza kasi katika jitihada zao za kutaka kushinda.
Mechi hii ni sehemu ya mashindano makubwa ya CAF Confederation Cup, na inaongeza msisimko kwa wapenzi wa soka katika Afrika nzima.
Huku mashabiki mbalimbali wakisema “Wakati tunapoingia uwanjani, tunawakilisha taifa letu na tunavalia jezi zetu kwa heshima kubwa. Kila pasi, kila shambulio, na kila ulinzi una umuhimu mkubwa”.
Muda wa mechi, saa 3:30 PM (E.A.T), unakaribia haraka. Mashabiki wanaohudhuria uwanjani na wale wanaotazama kutoka kwa runinga watakuwa na hamu kubwa ya kuona jinsi timu yetu itavyofanya. Tunawaomba mashabiki wetu waaminifu kuja kwa wingi na kutupa sapoti ili kuwapa nguvu wachezaji wetu.
Tunajivunia kuwa sehemu ya CAF Confederation Cup na tuko tayari kushindana na timu yoyote. Hii ni fursa yetu ya kuonyesha vipaji vyetu na kuwapa furaha mashabiki wetu. Tumejiandaa vizuri, na tuko tayari kwa changamoto. Acha siku ya mechi ije, na tutashinda kwa pamoja!
Tutakapokutana uwanjani na Bahir Dar Kenema, tutacheza kwa moyo na kwa umakini, tukilenga kuleta ushindi nyumbani. Tuna imani kubwa katika timu yetu na mashabiki wetu waaminifu. Twende tujivunie soka letu na tuifanye siku hii kuwa ya kumbukumbu.
Usikose kufuatilia mechi hii kubwa katika dimba la ABEBE BIKILA saa 3:30 PM (E.A.T). Twende tuiunge mkono timu yetu, tukiwa na matumaini ya ushindi!”
Tambo ni nyingi sana kuelekea mchezo huu.
#KonceptTvUpdates