Azam FC imetupwa nje ya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika kwa penati 4-3 kufuatia matokeo ya jumla kuwa sare ya 3-3 dhidi ya Bahir Dar Kenema ya Ethiopia.
Hii ni baada ya mchezo wa marudiano kuchezwa jana kwenye dimba la ChamazI na Azam kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 ndani ya dakika 90 na baadae kuamliwa kwa mikwaju ya penati, ambapo Bahir Dar walishinda kwa mikwaju 4 na Azam fc kupata mikwaju 3 kati ya mitano.
Ikumbukwe kuwa mchezo wa awali uliochezwa nchini Ethiopia wiki moja iliyopita Azam alipoteza kwa kipigo cha bao 2-1 katika mchezo wa kwanza.
Azam alikuwa ni mwakirishi wa Tanzania bara kwenye mashindano ya kombe la shirikisho barani Afrika Pamoja na Singida Fountain Gate fc.
#KonceptTVUpdates