ADVERTISEMENT
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
Saturday, September 23, 2023
  • Login
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
No Result
View All Result

Benki ya NMB yadhamini Maonesho ya Nane Nane kwa Shilingi Mil. 80/-

I am Krantz by I am Krantz
Aug 1, 2023
in HABARI, MICHEZO
0
Benki ya NMB yadhamini Maonesho ya Nane Nane kwa Shilingi Mil. 80/-
0
SHARES
64
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Juma Homera ( wa kati mstari wa mbele) akifurahia pamoja na kamati ya maandalizi ya Maonesho ya Kilimo Nane Nane ya Mkoa wa Mbeya pamoja na Maafisa wa NMB, baada ya kupokea mfano wa hundi ya Shilingi milioni 80 kutoka kwa Kaimu Meneja wa NMB Kanda ya Nyanda za Juu – Frank Rutakwa (watatu kushoto) kama udhamini wa Benki ya NMB kwa maonesho hayo yanayoanza leo jijini Mbeya.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Juma Homera (kulia) akipokea mfano wa hundi ya Shilingi milioni 80 kutoka kwa Kaimu Meneja wa NMB Kanda ya Nyanda za Juu – Frank Rutakwa kwa ajili ya udhamini wa Benki ya NMB katika maonesho ya Kilimo Nane Nane yanayofanyika Kitaifa Mkoani Mbeya.

Kwa kuthamini mchango wa kilimo katika ukuaji wa uchumi nchini, Benki ya NMB imedhamini Maonesho ya Nane Nane kwa kutoa shilingi milioni 80. Maonesho haya makubwa ya wakulima Nane Nane yanatarajiwa kuzikutanisha zaidi ya nchi 30 na kitaifa yanafanyika Jijini Mbeya kuanzia leo tarehe moja hadi tarehe Nane mwenzi huu.

Akikabidhi mfano wa hundi ya kiasi hicho cha fedha, kwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Kaimu Meneja wa Kanda Nyanda za Juu – Frank Rutakwa amesema kwa kipindi cha miaka sita cha maonesho hayo ambayo yamekuwa yakifanyika Kitaifa mkoani Mbeya, Benki hiyo imedhamini jumla ya Shilingi Milioni 255.

RelatedPosts

Maurel and Prom: Empowering Tanzania’s Sustainable Energy Economy

Maurel and Prom: Empowering Tanzania’s Sustainable Energy Economy

Sep 22, 2023

DR KONGO YATAKA MONUSCO KUONDOKA HARAKA

Sep 21, 2023

HAIER TANZANIA NA AZAM TV WAUNGANA KUKIWASHA KWA PAMOJA

Sep 21, 2023
Load More

Aliongeza kuwa, NMB imeweka idara maalumu ya Kilimo na Mameneja Uhusiano kwenye kila Kanda ili kuhakikisha kilimo kinafanikiwa na kinakuwa msingi imara kwa uchumi wa nchi yetu. Aidha, alisema kuwa ndani ya miaka minne, wamefungua zaidi ya akaunti 644,034 za wakulima nchi nzima. Mwaka huu kwa Mkoa wa Mbeya pekee, wamefanikiwa kufungua akaunti zaidi ya 87,044 za wakulima wa kahawa, mpunga, parachichi, mahindi nk.

Bw. Rutakwa alibainisha kuwa kupitia NMB Foundation, NMB imeweza kutoa elimu ya fedha na mfunzo ya biashara kwa vyama vya ushirika vya wakulima (AMCOS) 1,450 nchi nzima, ili kuwajengea uwezo wa namna bora ya kusimamia mapato yao. Huku kwa Nyanda za juu pekee wameshirikiana na AMCOs zaidi ya 555 zilizopo Mbozi (kahawa), Rukwa (Mahindi, Soya na Ufuta), Chunya (Tobacco), Njombe (Viazi Ulaya)
Akizungumza mara baada ya kupokea mfano wa hundi ya shilingi milioni 80 kutoka Benki ya NMB, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya-Mhe. Juma Homera aliishukuru Benki ya NMB kwa msaada huo na kwa kuendelea kuwa karibu na wakulima kwa kuwasaidia pembejeo na Matrakta hivyo kusidia kukuza sekta ya kilimo nchini.

“Benki ya NMB ni mojawapo ya taasisi za kifedha zinazoongoza nchini kwa kuchangia kwa dhati juhudi za serikali katika kukuza kilimo, ufugaji, uvuvi na sekta zingine hususani za Elimu na Afya ambazo wamekuwa mstari wa mbele kutoa michango mara kwa mara,” Alisema Mkuu huyo wa Mkoa.

Related

I am Krantz

I am Krantz

👉 FOUNDER & CEO of KONCEPT 👉Serial & Self-made Entrepreneur 👉Digital media consultant 👉Pr & media Guru/Awards winner Blogger 👉Startuper of the year 2016 by TOTAL 👉TOP 50 Most influential young Tanzania 2017 👉General Secretary at Tanzania Bloggers Network 👉 UPG Sustainability Leader in the Class of 2021 👉 ALUMNI The Tony Elumelu Foundation 👉Chairman YOUNG CEO CLUB Tanzania 🇹🇿 ‘ 😊 Marketer BY Education, Entrepreneur BY Profession & Blogger BY Passion ”😊

Related Posts

Maurel and Prom: Empowering Tanzania’s Sustainable Energy Economy
BIASHARA

Maurel and Prom: Empowering Tanzania’s Sustainable Energy Economy

by I am Krantz
Sep 22, 2023
DR KONGO YATAKA MONUSCO KUONDOKA HARAKA
HABARI

DR KONGO YATAKA MONUSCO KUONDOKA HARAKA

by SUZO SHUKRANI
Sep 21, 2023
HAIER TANZANIA NA AZAM TV WAUNGANA KUKIWASHA KWA PAMOJA
HABARI

HAIER TANZANIA NA AZAM TV WAUNGANA KUKIWASHA KWA PAMOJA

by SUZO SHUKRANI
Sep 21, 2023
MNH YAFANYA UPASUAJI WA KWANZA TUNDU DOGO MOJA
AFYA

MNH YAFANYA UPASUAJI WA KWANZA TUNDU DOGO MOJA

by SUZO SHUKRANI
Sep 21, 2023
SBL KUUNGANISHA TAMADUNI KUPITIA OKTOBA FEST
HABARI

SBL KUUNGANISHA TAMADUNI KUPITIA OKTOBA FEST

by SUZO SHUKRANI
Sep 21, 2023
TAWA YATAKIWA KUJIPANGA KUONGEZA UKUSANYAJI MAPATO
HABARI

TAWA YATAKIWA KUJIPANGA KUONGEZA UKUSANYAJI MAPATO

by SUZO SHUKRANI
Sep 21, 2023

KRANTZ MWANTEPELE (FOUNDER & CEO)

KONCEPT TV

https://www.youtube.com/watch?v=0HP0mB_rtIU&t=7s
KONCEPT TV

KONCEPT TWEETS

August 2023
M T W T F S S
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
28293031  
« Jul   Sep »
Currently Playing
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In