DAKTARI Bingwa wa Magonjwa ya Mfumo wa Mkojo na Uzazi wa wanaume katika Hospitali ya Rufani ya Benjamin Mkapa, Remigius Rugakingira, amesema waendesha bodaboda wanaobeba abiria kwa mtindo wa mishikaki na kukalia tangi la mafuta, wako hatarini kupoteza nguvu za kiume.
“Kwanza mafuta yenyewe ni kemikali. Tangi linaloyahifadhi hupata joto pikipiki ikitembea kwa muda mrefu, hivyo kwa mwendeshaji kukaa juu yake maana yake hupokea joto hilo kwenye korodani ambayo ni kiwanda cha kuzalisha mbegu za uzazi na vichocheo vinavyochangia uume kusimama,” alisema Dk. Rugakingira
Dk. Rugakingira aliyasema hayo jijini Dodoma akieleza kuwa madereva hao wako hatarini kukabiliwa na upungufu wa nguvu za kiume siku za usoni kwa sababu ya kukalia matangi hayo ambayo hupata joto baada ya pikipiki kutembea mwendo mrefu.
Mtaalam huyo analitaja kundi lingine lililo hatarini ni vijana wanaovaa nguo za kubana (skin jeans), na nguo za ndani (boxers) zinazobana korodani kuwa hawapo salama ikiwa wataendelea na tabia hizo kwa muda mrefu.
#KonceptTVUpdates