Bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania limeanza rasmi vikao vya mkutano wa kumi na mbili ambapo hii inakuja mara baada ya taarifa kutolewa rasmi na bunge juu ya ratiba yake ya vikao.
Ikumbukwe kuwa bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania liliahirisha vikao vyake mwezi juni tarehe 28 na Waziri mkuu Kassim Majaliwa.
Vikao hivi vya bunge vinatarajiwa kudumu kwa takribani majuma mawili ambapo tarehe rasmi ya kuahirishwa kwa vikao vyake itakuwa ni septemba 8 kulingana na ratiba iliyotolewa na bunge.
#KonceptTVUpdates