MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila amesimamisha kuanza kwa soko jipya la Mbagala Zakhiem kwa muda wa siku saba ili afanye uchunguzi kubaini waliotoa fedha kwa madalai ili wapatiwe maeneo ya kufanya biashara ndani ya soko hilo.
Chalamila ametoa kauli hiyo jana tarehe 28, Augosti mbele ya viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Temeke na wananchi baada ya kuzindua soko hilo jipya ambalo ujenzi wake umegharimu kiasi cha sh.bilioni 2.2 ambapo ameeleza pamoja na kulizindua na kutakiwa kuanza kufanya kazi leo, amesitisha kwa muda uzindizi huo kwa ajili ya kufanya uchunguzi.
“Kama umeliwa fedha yako kwa kuambiwa utapata eneo kwenye soko hili ukitoka hapa kamwabie uliyempa Chalamila kasema nirudishie hela yangu kwasababu hapo sitapata.Mimi moja ni moja na mbili ni mbili sitakuficha, na madalali wa aina hiyo wapo , wapo ambao si watumishi wa umma na wapo watumishi wa umma
“Nimesema kwenye utawala ambao mimi nipo hapa ni Mkuu wa Mkoa kwa leo ni lazima watu tuwe na nidhamu na adabu ya kufuata misingi ili mambo yaende vizuri.
“Asitokee hata mmoja kujiona yeye ni dalali mzuri , mimi nitakunyoosha vizuri hata kama ni dalali wa miaka mingi.Tunahitaji watu waelewe kwamba kama hili soko linakwenda kwa utaratibu gani.
Alibainisha kuwa soko hilo lililogharimu zaidi ya sh 2 bilioni lina maduka 150 lakini wafanyabiashara waliotuma maombi ni zaidi ya 2000.
“Nitakapokamilisha uchunguzi nitahakikisha bei ya pango inaenda na hadhi ya soko, nitatoa utaratibu kuhakikisha makundi yote wanapata nafasi wakiwemo walemavu na vijana,”ameongeza.
“Awe Diwani, awe nani, awe Mwenyekiti, awe ni dalali nitapita naye kwenye mkanda mmoja namna hii kwasababu Rais wetu Dk.Samia Suluhu Hassan ametoa Sh.bilioni 2.2 kwa ajili ya ujenzi wa soko la Zakhem.
“Zimetolewa kwa ajili ya ujenzi wa soko hilo na hakuna mtu aliyechangishwa kujenga soko hilo.Na nitakapokamilisha uchunguzi huo tutangalia saa na bei ya pango ambayo itakwenda kulingana na thamani ya ujenzi wa soko.
#KonceptTVUpdates