Baada ya ukimwa wa mrefu hatimaye Clara Luvanda atimkia nchini Hispania kukipiga kwenye timu ya DUX Logrono fem inayoshiriki ligi ya wanawake nchini humo.
Ikumbukwe kuwa Clara Luvanda alikuwa akikipiga kwenye klabu ya Yanga princess na timu taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17 iliyoshiriki michuano nchini Cameroon.
Luvanda amekuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu kiasi cha mashabiki wengi kuhoji kulikoni juu kutoonekana kwa mchezaji huyo akikiwasha uwanjani.
Bado haijawekwa wazi kuwa amesajiliwa kwa muda gani kwa timu hiyo ya nchini Hispania.
#KonceptTVUpdates