Katika kuelekea kilele cha siku ya maonesho Nane Nane nchini, Makamu wa Rais, Dk. Philip Mpango amesisitiza ushirikishwaji wa kifedha kufanyika Katika jukwaa la maonesho ya Kilimo NaneNane.
Aidha, Makamu wa Rais Dk Philip Mpango amezitaka taasisi za fedha nchini kutumia vyema Maonesho ya Kilimo ya NaneNane ili kuwa jukwaa la kutoa elimu muhimu ya fedha kwa wakulima. Aliipongeza Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) kwa kuanzisha banda maalumu la kutoa maarifa hayo muhimu. Mtazamo wa ujumuishaji wa kifedha unalenga kuwawezesha wakulima na kuongeza uelewa wao wa masuala ya kifedha kwa ukuaji endelevu wa kilimo.”
#mwanahalisi
#KonceptTvUpdates